Pages

Thursday, December 20, 2012

Kesi ya ya Viongozi wa Uamsho yatupwa


Written by    20/12/2012
MAHAKAMA Kuu ya Zanzibar imetupilia mbali kesi ya viongozi wa Uamsho waliokuwa wanadai kunyimwa huduma muhimu wakiwa mahabusu. Jaji Mkusa Isaack Sepetu jana aliitupa kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2012 iliyofunguliwa dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP), Ibrahim Mzee Ibrahim, Novemba 8 mwaka huu.

Jaji Sepetu alisema kwamba kesi hiyo iliyofunguliwa na wakili Abdallah Juma Mohammed imefunguliwa kinyume na kifungu cha 4 sura ya 28 cha Sheria za Mawakili na Wanasheria ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Alisema nyaraka zimekosa jina la mtu aliyekula kiapo kwa niaba ya washitakiwa na kukosekana tarehe ya hati ya kiapo hivyo kuzifanya ziwe kinyume cha sheria. Alisema kimsingi mambo hayo hayakukidhi hoja za kisheria kwa hivyo anaitupa kesi hiyo iliyofunguliwa na viongozi wa Uamsho.
Viongozi wa Uamsho walifungua kesi hiyo wakidai kwamba hawatendewi haki katika mahabusu ya Kiinua Maguu iliyopo Zanzibar kwa kunyimwa haki za kubadilisha nguo, kuabudu, kuonana na jamaa zao na zingine.
Wakili wa washitakiwa hao, Salum Toufioq alisema kwamba wateja wake sasa wanapewa huduma hizo lakini hawajaruhusiwa kuonana na jamaza zao tangu kesi hiyo ilpoanza. Jaji Mkussa alisema kwa mujibu wa sheria ya Vyuo vya Mafunzo Zanzibar washitakiwa hao wana haki ya kupewa huduma zote sawa na mahabusu wengine.
Kesi ya msingi inayowakabili viongozi hao wa uamsho itaendelea Januari 3 mwakani. Viongozi wa Uamsho waliofikishwa mahakamani ni Masheikh Farid Hadi Ahmed, Msellem Ali Msellem, Azzan Khalid Hamdan, Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Khamis Ali Suleiman na Hassan Bakari Suleiman.

No comments:

Post a Comment