Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim
Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Waziri katika Wizara ya Mambo ya Nje
ya Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika na Jumuiya ya Madola,
Bw. Mark Simmonds, katika makao makuu ya Wizara ya mambo
ya Nje (Foreign and Commonwealth Office), mjini London, nchini
Uingereza. Katika mazungumzo hayo, Maalim Seif hakutafuna maneno
kuhusiana na mwelekeo wa matakwa ya Wazanzibari kutaka kuirejesha
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa
ikiwa na kiti chake Umoja wa Mataifa (UN) ambayo itaingia katika
mashirikiano ya Mkataba na Jamhuri ya Tanganyika. Pamoja Daima!
No comments:
Post a Comment