Pages

Thursday, December 20, 2012

ICC yapokea malalamiko ya LHRC polisi kuua raia


Written by   20/12/2012 
Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimejibiwa rasmi barua kiliyoandika katika Mahakama ya Kimataiafa ya Uhalifu (ICC), iliyopo The Hague nchini Uholanzi ambayo inalenga kulifikisha Jeshi la Polisi nchini kwenye mahakama hiyo kutokana na kuendelea kuwaua raia wasiokuwa na hatia.
Mkurugenzi wa LHRC, Dk. Hellen Kijo-Bisimba, amesema barua waliyojibiwa hivi karibuni na ICC, ni miongoni mwa maombi mengi waliyowasilisha katika vyombo vingine vya kimataifa kuviomba vichunguze uhalifu unaofanywa na Jeshi la Polisi hapa nchini dhidi ya raia.
Dk. Bisimba aliyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.
Hata hivyo, Dk. Bisimba alisema licha ya Polisi kuendelea kuwaua raia, kituo chake kinalaani mauaji yaliyofanywa na raia dhidi ya Polisi wawili wiki iliyopita mkoani Kagera.
Wiki iliyopita, Polisi wawili waliuawa na raia wenye hasira baada ya Polisi hao kumuua raia kwa risasi wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
Hadi sasa, watu 40 wanashikiliwa na polisi kuhusiana na mauaji hayo.
Akizungumzia uhalifu unaofanywa na Polisi hapa nchini, Dk. Bisimba alisema wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu, lakini mwaka huu matukio ya mauaji yanayofanywa na chombo hicho yamezidi kuongezeka.
“Tumejibiwa rasmi barua tuliyoandika kwa Mwendesha Mashitaka wa ICC na ameahidi kuifanyia kazi ikiwemo kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli kwa lengo la kuchukua hatua nyingine,” alisema Dk. Bisimba.
Alifafanua kuwa kinachochangia kuwapo mauaji kwa mwaka huu, ni ukosefu wa utawala wa sheria ulionyooka hapa nchini, hatua ambayo raia na Polisi kila mmoja anamuona mwenzake kama adui.
Kwa upande wa raia kuwaua Polisi ama kuua raia mwenzao, Dk. Bisimba alisema suala hilo linaweza kushughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi na vyombo vya usalama.

Kesi ya ya Viongozi wa Uamsho yatupwa


Written by    20/12/2012
MAHAKAMA Kuu ya Zanzibar imetupilia mbali kesi ya viongozi wa Uamsho waliokuwa wanadai kunyimwa huduma muhimu wakiwa mahabusu. Jaji Mkusa Isaack Sepetu jana aliitupa kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2012 iliyofunguliwa dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP), Ibrahim Mzee Ibrahim, Novemba 8 mwaka huu.

Friday, September 14, 2012

Maalim Seif ziarani UK

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Waziri katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika na Jumuiya ya Madola, Bw. Mark Simmonds, katika makao makuu ya Wizara ya mambo ya Nje (Foreign and Commonwealth Office), mjini London, nchini Uingereza. Katika mazungumzo hayo, Maalim Seif hakutafuna maneno kuhusiana na mwelekeo wa matakwa ya Wazanzibari kutaka kuirejesha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa ikiwa na kiti chake Umoja wa Mataifa (UN) ambayo itaingia katika mashirikiano ya Mkataba na Jamhuri ya Tanganyika. Pamoja Daima!